TUKO.co.ke inakuletea makala fupi ya jinsi ya kupika, na hapa utajifunza juu ya kupika au kuandaa vyakula mbalimbali kuanzia hatua ya kwanza hadi mwisho.
Leo utajifunza jinsi ya kutengeneza mandazi na kama ijulikanavyo chakula hiki ni moja ya vitafunwa bora kabisa wakati wa asubuhi na watu wengi hupendelea kula, hii ni kutokana na ladha yake tamu na nzuri ambayo haikinaishi kama vyakula vingine vinavyoliwa asubuhi.

Viungo

Pia soma
Mamake Rex Kanyike Asimulia Nyakati za Mwisho za Mwanawe Kabla ya Kifo: "Wenzake Ilibidi Wakimbie"
MAKINIKA: Watumie wahariri wetu taarifa yako unayoiona kuwa bora! Tafadhali wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
MAANDALIZI

- Chekecha unga kwa kutumia chungio kwenye chombo utacho kandia unga wako.
- Chukua kikombe weka hamira, sukari vijiko 2, unga vijiko 2 na iache kwa dakika 5 mpaka ifure.
- Chukua unga ulio uweka kwenye chombo chako,weka baking powder,chumvi,sukari,hiliki na custard kisha changanya vizuri.
- Chukua hamira iliyoumuka changanya na unga wako kisha weka tui lako kidogo kidogo na uanze kuukanda.
- Kanda unga wako kwa dakika 10 mpaka uwe laini kisha uuache kwa muda wa dakika 5.
- Ongeza samli na uendelee kuukanda unga kisha uweke kwenye bakuli na uufunike ili usipitishe hewa uache tena kwa muda wa dakika 10.
- Ukishaumuka kata madonge na uyasukume kwa kutumia unga mkavu upate duara kubwa kama chapati hivi, ila isiwe nene sana wala nyembamba sana. Kisha kata mandazi yako kwa umbo la pembe tatu ama upendavyo.
- Yaache mandazi yako yaumuke kwa dakika zisizopungua 10 hivi.

Pia soma
Patrick Kilonzo Mwalua: Mwanamume Mkenya Aliyewapa Wanyamapori Maji Wakati wa Kiangazi Afariki
JINSI YA KUYACHOMA KWA MAFUTA


Muhimu:
- Ili andazi lako liwe zuri na laini hakikisha unakanda unga wako mpaka uwe laini sana.
- Upe muda unga huo kutulia ili ulainike vyema zaidi.
- Acha unga wako aumuke vizuri ndio uyachome mandazi yako.
- Ukitaka andazi liwe na nyama ndani usisukume unga wako kuwa chapati jembamba wakati wa kukata vipande vya umbo linalokupendeza.
- Na ukitaka lisiwe na nyama ndani sukuma chapati ya wastani tu wakati wa kukata shape yako na acha liumuke sana.

Pia soma
Rigathi Gachagua Anyoonyewa Vidole Huku Ruto Akiwaita Wabunge Ikulu Kabla ya Kura ya Mswada wa Fedha
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaX51f5BmpKKrn6i2bq%2FOq6Weql2ftq%2B%2FyGawmmWbqr2qt8BmpJqmlJbHqnnLmqCnoV2jrm65wK2Ypq1encGuuA%3D%3D